Posts

ZANZIBAR YANG'AA UTALII KIMATAIFA.

Image
  Zanzibar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa onyesho kubwa la utalii la kimataifa ambalo litafanyika kwa siku mbili tarehe 23 na 24 mwezi febuary mwaka 2023 katka hotel ya  golden tulip  uwanja wa ndenge zanzibar. Lengo kuu la onyesho hilo ni kuhakikisha wanaifikia dunia na kuonesha zanzibar imefunguka ipo salama ili kuwahamasisha watatii kutoka mataifa mbalimbali kutembelea visiwani humo. Pia makampuni takribani 130 yanatarajiwa kuhudhuria onyesho hilo hadi sasa makampuni 95 tayari yamejisajili. ​

Dkt Samia amaliza kero ya maji Njombe

Image
Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe umeanza kutekeleza Mradi wa maji utakaonufaisha wakaazi 4,144 wa kijiji cha Vyombo Wilayani humo. Meneja wa Ruwasa wilaya ya Njombe ELIKALIA MALISEMA alisema lengo la kujenga Mradi huo ni kuwapunguzia Wananchi wa kijiji cha Vyombo adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji. Pia alisema mradi huo unafadhaliwa na Serikali ya Tanzania kwa Gharama ya sh 893,730,555 kupitia mfuko wa maji (NWF) ambapo muda wa utekelezaji wake ni miezi sita. Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Vyombo E ZEKIA MLINGULA , alimshukuru Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa mapenzi makubwa ya kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa maji utakaomaliza kero kubwa ya maji.   

Historia ya morocco

Image
 Historia Makala: Historia ya Moroko Moroko ya Kale Habari za kimaandishi za kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani lilibaki nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale (usiuchanganye na nchi ya kisasa Mauretania) uliounganisha sehemu kubwa ya Moroko ya kaskazini. Wamauretania wa kale walishirikiana na Dola la Roma hadi kuwa jimbo la dola hili kwa jina la "Mauretania Tingitana". Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Roma kuanzia mwaka 400 BK kukawa na uvamizi wa Wavandali. Uvamizi wa Kiarabu Karne ya 7 BK ilileta uvamizi wa Waarabu walioteka nchi na kusababisha polepole Waberber (waliokuwa Wayahudi, Wakristo au wafuasi wa dini za jadi) kuwa Waislamu. Mwanzoni Moroko ilikuwa sehemu ya milki ya khalifa ya Waomawiyya waliotawala Dameski (Siria). Baada ya kupinduliwa kwa Waomawiyya na Waabasiya wa Baghdad (Iraq) mkimbizi Mwarabu Idris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea.

WALIOGOMA KUHAMA NGORONGORO WAJUTA

Image
  Ukame na njaa inayoendelea kutikisa mkoa wa Arusha na baadhi ya maeno nchini umewafanya wananchi waliokataa kuhama kwa huyari kutoka Bonde la Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomero katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga wajuta. mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,  RAYMOND MANGWALA  alisema kutokana na ukame wa muda mrefu idadi ya mifugo inayokufa Wilayani humo imeongezeka ikilinganishwa na kipindi kilichopita. Pia alisema suluhisho la wafugaji wa Ngorongoro ni kwenda katika maeneo yenye miundombini imara ya malisho na maji yaliyojengwa na Serikali Msomera Wilaya Handeni. katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni  MASHAKA MGETA  Alisema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo ya malishio kwa wafugaji wa Msomera na Handeni kwa ujumla yameongezeka na kufanya wafugaji kusahu kupoteza mifugo yao kutokna na ukosefu wa malisho na maji. Pia Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Msomera kata ya misima,  MARTIN OLEIKAYO  aliishukuru serikali kwa kuwajengea wafugaji miundo mbinu rafiki.

YAMETIMIA UMEME BWAWA LA NYERERE

 Mradi wa kufua umeme  bwawa la mwalimu julius nyerere (JNHPP) umekamilika kwa asilimia 78.68 huku hatua ya kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji ikiwa imefikiwa kwa lengo la kuruhusu ujazaji wa maji katika bwawa tayari kwa umeme kuanza kuzalishwa. Hata hivyo itafuatiwa na kuashwa mitambo baada ya kujaa kwa bwawa hatua ambayo inatarajiwa kuchukua misimu miwili ya mvua . Bwawa hilo linatarajiwa kukamilika na kuanza uzalishaji juni mwaka 2024 litagharimu sh trilioni 6.5 hadi kukamilika kwake.Bwawa hilo linaukubwa wa meta za ujazo 32.3. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 2115 zitakazoengeza nguvu katika megawati 1500 zinazozalisha vyanzo mbali mbali vya sasa na kuondosha kwa mahitaji yake ya umeme na kuwa na ziada ya kuuzwa nchi jirani sambamba na kupunguza gharama za umeme kwa watanzania