Dkt Samia amaliza kero ya maji Njombe

Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe umeanza kutekeleza Mradi wa maji utakaonufaisha wakaazi 4,144 wa kijiji cha Vyombo Wilayani humo.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Njombe ELIKALIA MALISEMA alisema lengo la kujenga Mradi huo ni kuwapunguzia Wananchi wa kijiji cha Vyombo adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji.

Pia alisema mradi huo unafadhaliwa na Serikali ya Tanzania kwa Gharama ya sh 893,730,555 kupitia mfuko wa maji (NWF) ambapo muda wa utekelezaji wake ni miezi sita. Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Vyombo EZEKIA MLINGULA, alimshukuru Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa mapenzi makubwa ya kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa maji utakaomaliza kero kubwa ya maji. 







 

Comments

Popular posts from this blog

ZANZIBAR YANG'AA UTALII KIMATAIFA.

Historia ya morocco