YAMETIMIA UMEME BWAWA LA NYERERE

 Mradi wa kufua umeme  bwawa la mwalimu julius nyerere (JNHPP) umekamilika kwa asilimia 78.68 huku hatua ya kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji ikiwa imefikiwa kwa lengo la kuruhusu ujazaji wa maji katika bwawa tayari kwa umeme kuanza kuzalishwa.

Hata hivyo itafuatiwa na kuashwa mitambo baada ya kujaa kwa bwawa hatua ambayo inatarajiwa kuchukua misimu miwili ya mvua .

Bwawa hilo linatarajiwa kukamilika na kuanza uzalishaji juni mwaka 2024 litagharimu sh trilioni 6.5 hadi kukamilika kwake.Bwawa hilo linaukubwa wa meta za ujazo 32.3.

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 2115 zitakazoengeza nguvu katika megawati 1500 zinazozalisha vyanzo mbali mbali vya sasa na kuondosha kwa mahitaji yake ya umeme na kuwa na ziada ya kuuzwa nchi jirani sambamba na kupunguza gharama za umeme kwa watanzania

Comments

Popular posts from this blog

Dkt Samia amaliza kero ya maji Njombe

ZANZIBAR YANG'AA UTALII KIMATAIFA.

Historia ya morocco